Wanagombea mifupa


Kuna shule kutembea, waliyanena
Wala sikutegemea, nilo yaona
Mifupa wana gombea, si nyama tena.

Kachinjwa ng’ombe mzima, na waungwana,
Watu wanaacha nyama, iliyonona,
Mifupa wana gombea, si nyama tena.

Walaji wakajongea, wa kila kona
Kimbembe kikatokea, kusukumana
Mifupa wana gombea, si nyama tena.

Author: Gadi Solomon