Gadi Solomon, Swahili Hub
Dar es Salaam. Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kupitia Baraza la Kiswahili la Taifa (Bakita) kwa kushirikiana na Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kupitia Mamlaka ya Mawasilinao Tanzania (TCRA) wametangaza kongamano la nne la idhaa za kiswahili ambalo kwa mwaka huu litafanyika jijini Mbeya.
Katika Bakita imeeleza kwamba kongamano hilo litawahusisha watangazaji wa redio, television, watozi wa studio zote za muziki, filamu, matangazo, waandishi wa habari, wahabarishaji mtandaoni na maofisa habari wa wizara, idara, taasisi za serikali na kampuni na mashirika.
Kongamano hilo linatarajiwa kufanyika kuanzia Machi 18 hadi 22 mwaka huu katika HotelI ya Eden Highlands jijini Mbeya likiwa na Kaulimbiu “Tasnia ya habari na fursa za ubidhaishaji Kiswahili duniani”.
Kongamano la Idhaa za Kiswahili Duniani kwa mwaka jana lilifanyika visiwani Zanzibar na mada mbalimbali ziliwasilishwa na wataalamu wa lugha ya Kiswahili.
Kongamano hilo liliandaliwa na Baraza la Kiswahili la Zanzibar (Bakiza) kwa kushirikiana na wadau wengine, lilkiwakutanisha waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari vya kimataifa na wadau wengine wa lugha ya Kiswahili ikiwa ni pamoja na vyuo Vikuu.
Katika hotuba ya ufunguzi wa kongamano hilo hapo jana, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Mwinyi aliwataka washiriki watumie vyema taaluma zao katika utangazaji na uandishi wa habari.
Miongoni mwa mada zilizowasilishwa katika kongamano hilo ni “Changamoto za Matumizi ya Kiswahili katika kazi ya utangazaji ndani ya vituo vituo vya kazi”.
Maoni Mapya