Ya mkiwa haizai nyike

Na Pelagia Daniel

  1. Ya tanaki si ya tundwi, methali hii ina maana ya Tanaki katika methali hii ni debe kama lile litiliwalo samli, na tundwi ni mtungi ukaao nyumbani unaotiwa maji. Maji yaliyomo katika debe si kama yale yaliyomo mtungini, ya kwenye debe kwa desturi huwa ya moto, ya kwenye mtungi huwa ya baridi. Methali hii hutumiwa kuonyesha kwamba mke uliyenaye nyumbani huna wasiwasi naye tofauti na wa nje.
  2. Ya mkiwa haizai nyike, Mkiwa maana yake ni maskini na makusudio ya mkiwa ni ng’ombe wa maskini. Methali hii ina maana ya ng’ombe wa maskini hazai ng’ombe mke kwa kuwa ng’ombe mke atazaa na hivyohuyo maskini atabariki, akibariki hatakuwa maskini tena.
  3. Visima vya kale havifukiwi, methali huu ina maana si vizuri kuvifukia visima vya zamani huenda siku mojsa vikafaa. Ni sawa na kuwathamini wazee kwa sababu maarifa waliyonayo ni mengi, kwa hiyo wakati wowote wanaweza kutufaa.

Author: Gadi Solomon